Baada ya Waziri wa Mambo ya Nje wa China kutua kijijini kwa Rais Magufuli, Chato, katika ziara yake wiki iliyopita, Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi nae atawasili kesho kijijini hapo kwa ziara ya siku mbili. Yayumkinika kuiangalia Chato sasa kama “Ikulu isiyo rasmi” baada ya shughuli mbalimbali za kiserikali kuhamia katika kijiji hicho.
