Categories
Habari Siasa

Serikali ya Mama @SuluhuSamia Yawarejesha Kazini Watumishi Zaidi ya 4,000 Walioondolewa Kipindi cha Utawala wa Magufuli kwa Madai ya Kugushi Vyeti

Serikali kupitia Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala bora imetangaza kuwarejesha kazini Wafanyakazi zaidi ya elfu nne (4000+) ambao waliondolewa kazini kutokana na kugushi vyeti katika maeneo mbalimbali lakini sasa kwa huruma ya Rais Samia watarejeshwa kazini kwa sharti la kuwa wawe wamejiendeleza kielimu.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala bora Mohamed Mchengerwa amesema “wale walioweza kujiendeleza ambao ni zaidi ya 4100 tayari wamerejeshwa kazini, pia tunao Watumishi 1150 ambao hawakufanikiwa kujiendeleza maana yake hawana sifa za kutosha kuendelea kuitumikia Serikali japo walikua ni Watendaji wazuri.”