Categories
Habari Siasa

Mbowe Amtetea Sabaya, Asema Ametolewa Kafara Na Mama Samia Huku Wahalifu Wengine Kama Waliotaka Kumuua Lissu Wakidunda Mtaani.

Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe, amesema serikali ya Rais Samia Suluhu imeamua kumtoa kafara aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya na kuwaacha wahalifu wengine ikiwemo waliompiga risasi Lissu wakidunda serikalini bila kukamatwa.


Mbowe amesema kitendo cha Rais Samia kukataa kukutana na viongozi wa Chadema kwa miezi minne sasa ni cha kinyama na hawawezi kuvumilia hivyo kuanzia sasa hatampigia magoti tena kumuomba wakutane nae mbali watakutana barabarani.