Categories
Habari Siasa

Mama Samia Awataka Watanzania Wadumishe Amani, Asema “Vijichokochoko Vimeshaanza.”

Niwaombe sana tulinde amani, vijichokochoko vimeanza naomba msivipokee, wanaokuja na vijichokochoko walishajua matumbo yao yanajaaje, chakula chao wanatoa wapi, pesa za matibabu watatoa wapi, nawaomba wasije wakawaingiza kwenye huo mkenge.

Pakichafuka ni wewe utakayekaa ndani na watoto wako na mama watoto na msijue chakula mnatoa wapi, msijue mtoto akiumwa mtakwenda kumtibu na pesa gani, niwaombe sana tulinde amani yetu, nchi yetu itulie tuendelee na maendeleo yetu.