Categories
Habari Siasa

Chadema Kufanya “Operesheni Haki” Nchi Nzima Kudai Katiba Mpya na Tume Huru Ya Uchaguzi, Yazindua “Chadema Digital App.”

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Taifa, tarehe 27 Mei 2021 siku ya Alhamisi, anatarajiwa kuzindua ‘Operesheni Haki,’ ambayo itafanyika nchi nzima.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Jumanne tarehe 25 Mei 2021 na Chadema, kupitia ukurasa wake wa Twitter, kampeni hiyo itazinduliwa jijini Arusha.

Taarifa ya Chadema imesema kuwa, lengo la operesheni hiyo ni kudai katiba mpya, tume huru ya uchaguzi, pamoja na uimarishwaji misingi ya haki nchini.

Sambamba na hilo, taarifa ya Chadema imesema, Mbowe ameendesha kikao cha Kamati Tendaji ya chama hicho, katika Kanda ya Kaskazini, kilichofanyika leo jijini Arusha.

“Leo Mei 25, 2021, Mwenyekiti wa chama Taifa, Freeman Mbowe, ameendesha Kikao cha Kamati Tendaji ya Kanda ya Kaskazini, jijini Arusha,” imesema taarifa ya Chadema.

Wakati huo huo, chama hicho kimezindua app yake kwenye Play store na App Store