Categories
Maoni

Magufuli Kuahidi Ndege 5 Zaidi Akishinda Urais Ni Kiburi na Kuwapuuza Watanzania Wanaolalamikia Ugumu wa Maisha

Kwamba hali ya maisha ya Watanzania ni ngumu, ni suala lisilohitaji utafiti wala mjadala. Kwamba ugumu huo umechangiwa na serikali kuwa na vipaumbele ambavyo hamvimnufaishi mwanachi wa kawaida moja kwa moja au hapo kwa hapo, nalo si jambo linalohitaji umahiri sana kulielewa. Ni wazi kuwa mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Rais aliyepo madarakani, John […]

Categories
Habari Siasa

Matumizi Mabaya Ya Fedha za Walipakodi: Magufuli Atuma Ndege Ya Rais Kwenda Kenya Kumleta Mchekeshaji

Rais John Magufuli, ambaye kwa miaka mitano ya utawala wake amekuwa akijinasibu kama anayechukia matumizi mabaya ya raslimali za umma, alitoa ndege ya rais kwenda Kenya kumleta mchekeshaji maarufu, Eric Omondi, kwa ziara ya siku mbili. Kwa mujibu wa taarifa za tovuti ya , licha ya serikali ya Tanzania kupiga marufuku ndege kutoka Kenya, msanii […]

Categories
Maisha Maoni Siasa

Uzinduzi wa Kampeni za CCM Dodoma: Makonda Azuiliwa Kwenda Kukaa Jukwaa La VIPs

Chama tawala CCM leo huko Dodoma kimezindua kampeni zake za uchaguzi mkuu kwa nafasi ya urais, ubunge na udiwani. Moja ya matukio yaliyogusa hisia za wengi katika uzinduzi huo ni kitendo cha wanausalama kumzuwia aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, kwenda kwenye jukwaa la wageni maarufu (VIP). Baadaye, kulisambaa picha inayomwonyesha […]

Categories
Michezo/Burudani

Simba Yaandika Historia: Sasa Inapatikana Kwenye “Gemu” ya Kompyuta ya Playstation

Klabu ya soka ya Simba ya Tanzania imeweka rekodi kwa kuwa ya kwanza Tanzania, na miongoni mwa chache barani Afrika, kuwemo kwenye “gemu” ya kompyuta (computer game) ya Playstation. Taarifa hizo ni kwa mujibu wa twiti ya mfadhili mkuu wa kalbu hiyo kongwe, Mohammed “Mo” Dewji.  

Categories
Siasa

Breaking News: Lissu Atangaza Maandamano Nchi Nzima Kushinikiza Tume ya Uchaguzi Kurejesha Wagombea wa Upinzani Walioenguliwa

Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chadema, Tundu Lissu, amewataka Watanzania kufanya maandamano ya amani nchi nzima kuishinikiza Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwarudisha bila masharti wagombea wa vyama vya upinzani walioenguliwa isivyo halali. Lissu ameongea hayo muda mfupi uliopita wakati anahutubia kwenye uzinduzi wa kampeni za urais, ubunge na udiwani kwa […]

Categories
Habari

Clouds TV na Radio Wafungiwa na TCRA kwa “Kutangaza Takwimu za Uchaguzi Ambazo Hazijathibitishwa na NEC.”

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imevifungia vituo vya habari vya Clouds TV na Radio kwa siku saba kuanzia kesho Agosti 28 na adhabu ya kuomba radhi siku nzima ya leo kwa kosa la kukiuka kanuni za utangazaji na kanuni ndogo za utangazaji za Uchaguzi. TCRA imesema kosa walilolifanya ni kutangaza takwimu za Uchaguzi ambazo hazijathibitishwa […]

Categories
Habari

Mchungaji Ashikiliwa na TAKUKURU kwa “Mikopo Umiza” Yenye Riba Hadi 200%

Mchungaji kiongozi wa Kanisa la Kiinjilisti la Kilutheri Tanzania wilayani Babati, Emmanuel Petro Guse, anashikiliwa na Taasisi ya Kuzuwia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa kuendesha biashara ya mikopo umiza bila ya kuwa na leseni ya biashara ya ukopeshaji fedha. Mkuu wa TAKUKURU Mkoani Manyara Holle Joseph Makungu akizungumza mjini Babati Agosti 28 amesema awali […]

Categories
Siasa

Uchaguzi 2020: Lissu Awawekea Pingamizi Magufuli Na Lipumba

Mgombea wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mhe. Tundu Lissu, amewawekea pingamizi wagombea wawili wa kiti cha urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Wagombea hao ni Dr. John Magufuli wa chama tawala CCM na Profesa Ibrahim Lipumba wa CUF. Hadi muda […]

Categories
Siasa

Licha Ya Ahadi Kuwa Wangeshirikiana, Lissu Na Membe Kila Mmoja Kugombea “Kivyake.”

Vyama vikuu vya upinzani nchini Tanzania vimeshindwa kuunda ushirikiano uliotarajiwa kuvisaidia vyama hivyo kumng’oa madarakani Rais John Magufuli katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 28 mwaka huu. Jana ilikuwa siku ya mwisho kwa wagombea wa nafasi ya urais kutoka vyama mbalimbali kurejesha fomu zao Tume ya Taifa ya Uchaguzi huko Dodoma, na baadaye Tume kutangaza wagombea […]

Categories
Habari

Video: Salamu Za Kiswahili Za Balozi Mpya Wa Marekani Tanzania, Vipaumbele Vyake Ni Pamoja Na Demokrasia, Haki Za Binadamu na Uhuru wa Habari