Uskochi imefuzu kushiriki mashindano ya nchi za Ulaya (Euro 2020) baada ya kuibwaga Serbia.
Hii ni mara ya kwanza katika miaka 22 kwa Uskochi kufuzu katika mashindano makubwa, mara ya mwisho ikiwa mwaka 1998.
Ryan Christie aliipatia Uskochi bao katika kipindi cha pili
kabla ya mshambuliaji wa Real Madrid, Luka Jovic kuisawazishia Serbia katika dakika za lala salama na kupelekea mechi hiyo kwenda muda wa nyongeza.
Hata hivyo, hakuna timu iliyoona nyavu katika dakika 30 za nyongeza na kupelekea penati.
Uskochi ilifanikiwa kuingiza nyavuni penati zote tano, wafungaji wakiwa Leigh Griffiths, Callum McGregor, Scott McTominay, Oli McBurnie and Kenny McLean.
Golikipa wa Uskochi David Marshall aliibuka shujaa baada ya kuokoa mkwaju wa tano wa Serbia uliopigwa na Aleksandar Mitrovic.
CHANZO: Sky News