Tetesi za usajili kwa vilabu vya soka hapa Uingereza zinadai kuwa mwanasoka pekee wa Tanzania katika Ligi Kuu ya England, Mbwana Samatta, yupo mbioni kujiunga na klabu ya Fenerbahce ya Uturuki kwa mkopo kutoka klabu yake ya sasa ya Aston Villa.

Hata hivyo kumekuwa na mkanganyiko kuhusu hatma ya mwanasoka huyo ambaye uwezo wake wa kufunga mabao hapo Aston Villa ni wa kuvutia.

Baba yake, Ally Samatta, amenukuliwa akisisitiza kuwa mwanae haendi popote na amemhakikishia kuwa atabaki England.