Categories
Michezo/Burudani

Mwanasoka Jake Daniels wa klabu ya Blackpool ya Uingereza atangaza kuwa ni shoga

Mwanasoka Jake Daniels wa klabu ya mpira wa miguu ya Blackpool ametangaza kuwa yeye ni shoga.

Hatua hiyo ya mwanasoka huyo wa timu hiyo inayokipiga kwenye ligi ya daraja la pili, ni ya kwanza baada ya zaidi ya miaka 30, ambapo mwanasoka wa zamani hapa Uingereza John Fashanu.

Daniels amesema kuwa amepata sapoti ya kutosha kutoka kwa familia yake, klabu na mashabiki wake baada ya kutanabaisha kuwa yeye ni shoga.

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson amempongeza mwanasoka huyo akisema amefanya ujasiri mkubwa na “ni hamasa kwa wengi.”

Licha ya ushoga kushamiri huku nchi za Magharibi, soka ni eneo ambalo halitarajiwi kuwa na mashoga japo kumekuwa na tetesi za muda mrefu kuhusu wanasoka wanaodhaniwa kuwa ni mashoga.