Categories
Michezo/Burudani

Miss Tanzania Rose Manfere Avuliwa Uwakilishi Kwenye Miss World, Badala Yake Ataenda Mshindi Wa Pili Juliana Rugumisa

Mrembo anayeshikilia tajia la Miss Tanzania 2020 -2021, Rose Manfere, amevuliwa uwakilishi wa kuiwakilisha nchi katika mashindano ya Dunia.

Hatua hiyo imechukuliwa na kamati ya Miss Tanzania baada ya kugundua baadhi ya tabia za mrembo huyo ambazo zitakuwa kikwazo cha kufanya vizuri katika mashindano hayo.

Taarifa za kuaminika zimeeleza kuwa:

“Mrembo ambaye anatakiwa kupata nafasi ya kuiwakilisha nchi anatakiwa awe na tabia njema kuanzia hapa nchi na kufuata kanuni na taratibu za mkataba wake nakwamba akikiuka kamati inatakiwa kuchukua hatua zinazostahili,” kimeeleza chanzo hicho.

Aidha, kimeongeza kuwa, nafasi hiyo amepewa mshindi wa pili wa Miss Tanzania 2020-2021 Juliana Rugumisa ambaye kamati imeona anafaa kuwa mwakilishi wa taifa.

Shindano la miss World mwaka huu linatarajiwa kufanyika nchini Puerto Rico mwishoni mwa mwaka huu.