Categories
Maoni

“Dear Mama Samia, Je Una Taarifa Za Changamoto Ya Mifumo Ya TEHAMA Hususan Kufeli Kwa Mfumo Wa Hazina Unaotoa Control Number?”

Anaandika mdau mmoja huko Jamii Forums

Ni takribani mwezi Sasa malipo ya serikali hayafanyiki kwenye taasisi mbalimbali baada ya kile kinachodaiwa mfumo wa hazina unaotoa control number kushindwa kufanya hivyo. Kutokana na changamoto ya control number fedha lazima zitakuwa zinapigwa kwa sababu huduma zinatolewa manually kitu ambacho Tulitangaziwa na Wizara ya fedha kimekwisha. Nimekwenda taasisi moja kuomba huduma nimekwamishwa na baada yakuwakomalia wakasema tatizo lipo nchi nzima.

Tatizo hili linatajwa kuchangiwa na wakandarasi wa mifumo yetu wasio Wazalendo na wasio na utaalamu wakutosha kufanya majukumu yao. Haiwezekani taasisi imalize wiki au wiki mbili haina internet au uwezo wa kutoa control number na hakuna taarifa kwa umma. Tutaamini vipi kwamba manualy way of payment pesa zinakwenda serikalini? Je,taasisi ambazo zimesitisha kutoa huduma kwa wateja wamekujulisha au wamekaa kimya wakisubiri uwazingue?

Nisingependa kutaja taasisi zinazolalamikiwa kukosa huduma lakini naamini ukiomba status ya taasisi utaelewa ninachosema hapa. Watu wameanza kufanya kazi wanavyojisikia.( Wizara ya fedha, maliasili, Kazi, bandari, mambo ya ndani, elimu, afya na uchukuzi hali si shwari kwenye huduma wanatoa manually kinyume na matakwa ya maelekezo yako yakurahisha huduma na kutumia tehama). Watu wanalalamika kuchelewa kwa huduma

Walianza Tanesco, watu wakapiga kelele mkarekebisha. Sasa hivi wamehamia taasisi nyingine zinazotoa huduma kwa control number. Waziri wa fedha amekaa kimya na Waziri wa mawasiliano amekaa kimya hadi watu walalamike ndipo waondoke ofisini wakajidai kutumbua watu.

Tatu, TTCL ni shirika la Taifa ila linakwenda kufa, kukosekana kwa hizi huduma serikalini zinachangiwa na TTCl kushindwa kutoa huduma. Je, Mhe. Rais hakuna watendaji TTCL wanapata kiasi flani Cha gawio kutoka makampuni ya simu ili wahujumu shirika then uwape tenda makampuni hayo? Je, waendeshaji wa TTCL wana vigezo?

Chanzo: Jamii Forums