Uamuzi wa mamlaka huko Ghana kumsimika “uchifu wa maendeleo” raia wa China Sun Qiang umepekelea malalamiko kutoka kwa baadhi ya wananchi.

Raia huyo wa China alisimikwa wadhifa ujulikanao kama Nkosuohene, ambao unamaanisha “chifu wa maendeleo” katika mji wa Kwahu Abetifi, mashariki mwa nchi hiyo.

Picha za “chifu” huyo wa Kichina akiwa amebebwa na wananchi zimepelekea mjadala mkali kwenye mitandao ya kijamii, ikiwa ni pamoja na kudhihaki kitendo hicho.