Categories
Habari

Zaidi ya Malori 150 ya Tanzania Yamezuiwa Kuvuka Mpaka Zambia. Baadhi ya Madereva Wadai Kusubiri Miezi Mitatu Sasa. Hali ni Kama Hiyo Huko Malawi.

Zaidi wa malori 150 ya Tanzania pamoja na madereva wake wazuiwa kuendelea na safari yao baada ya kuvuka mpaka na makontena ya magogo toka nchini DR Congo.

Tayari siku thelathini zimepita bila kupatikana ruhusa ya kuendelea na safari. Huku wengine pia wakisema wao wana siku 90 wamekwama nchini Zambia.

Madereva na wamiliki wa malori wamefanya juhudi kuwasiliana na ubalozi wa Tanzania mjini Lusaka Zambia na idara mbalimbali za serikali nyumbani Tanzania bila mafanikio.

Madereva hao wapo ktk kituo cha forodha mpakani nchini Zambia baada ya kuvuka na mzigo huo wenye nyaraka zote halali za mizigo na zinazoonesha wamiliki wa magogo ni wa Nchi DR Congo.

Maafisa wa forodha wa Zambia walidai kuwa magogo hayo ni ya kutoka nchini Zambia. Makontena yalifunguliwa na kufanyiwa uhakiki na kufungwa tena kwa seal lakini bado malori hayo ya Tanzania hayajaruhusiwa kuendelea na safari kuelekea bandari ya Dar es Salaam Tanzania.