Categories
Habari

Waliodai “Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Avujisha Video, Picha Zake Za Ngono” Wapandishwa Kizimbani, Video Husika Huko YouTube Ina “Views” Takriban Milioni Moja!

Hakimu Mkazi Kisutu, kujibu mashitaka ya kuendesha Chanel ya Utube bila kuwa na leseni.

Washitakiwa hao Adamu Thabit( 28) kutoka kampuni ya MMJ Steel Ltd na Mkurugenzi wa Bongo News YouTube, Heri Said(29).

Washitakiwa hao wamesomewa mashtaka yao na Wakili wa Serikali Mkuu, Nassoro Katuga akisaidiana na Faraja Ngukah, mbele ye Hakimu Mkazi Mwandamizi, Evodia Kyaruzi.

Alidai katika shtaka la kwanza ni kuchapisha maudhui yenye taarifa za uongo, ambapo washtakiwa wanadaiwa Juni 20, 2021 katika maeneo tofauti ya mkoa na jiji la Dar es Salaam, walichapisha picha na maelezo katika mfumo wa ujumbe mfupi wa maandishi uliosomeka” Ghafla Waziri Mkuu atumbuliwa, avujisha video picha zake za ngono” huku wakijua ujumbe huo ulikuwa ni wa uongo na ulikuwa na lengo la kupotosha umma.

Shtaka la pili ni kuendesha Chanel ya Utube bila kuwa na leseni, ambapo washtakiwa hao wanadaiwa kutenda kosa la kati ya Januari 2, 2018 na Julai 2, 2021 katika mkoa na jiji la Dar es Salaam, kupitia Chanel ya Utube yenye jina la Bongo News, walirusha maudhui kwenye mtandao yalikuwa na kichwa cha habari ” Ghafla waziri Mkuu atumbuliwa, avijsha video picha zake za ngono” bila kuwa leseni kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania.

Pia washitakiwa wanadaiwa kuchapisha maudhui yasiyoruhusiwa, ambapo inadaiwa Juni 20, 2021 katika jiji hilo, kwa makusudi walichapa maudhui yasiyoruhisiwa kupitia mtandano wa YouTube wa Bongo News, Maudhui ambayo yalionyesha picha za ngono zilizomhusisha waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Upande wa mashtaka ulidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika.

Washtakiwa wameshindwa kupata dhamana baada ya upande wa mashtaka kuiomba mahakama hiyo izuie dhamana kwa sababu za kiusalama.

Hata hivyo washtakiwa walipingana na hoja iliyotolewa na upande wa mashtaka wakidia kuwa siku Julai 2, 2021 walipopelekwa polisi walipata dhamana, na kuwa nje kwa dhamana na hakukuwa na tishio lolote la kiusalama.

Hakimu Kyaruzi baada ya kusikiliza hoja hizo alisema atatoa uamuzi kesho.

Hii ndo Video walipost ikiwa na kichwa cha habari “GHAFLA! WAZIRI MKUU ATUMBULIWA AVUJISHA VIDEO,PICHA ZAKE ZA NGONO”