Jana yalikuwa maadhimisho ya mwezi mmoja tangu alama ya reli #HabariNiMuhimuKulikoUbuyu izaliwe Mei 17 mwaka huu. Lengo la alama ya reli hiyo ni jitihada za kukabiliana na janga la ubuyu. Unaweza kuunga mkono jitihada hizo kwa kuritwiti twiti husika https://t.co/NWH1F4pCoN
— ๐๐๐ฌ๐ฎ๐ฌ๐ข (@Chahali) June 18, 2022
#HabariNiMuhimuKulikoUbuyu : Mwanajeshi wa kike Reut Rettig-Weissย amekuwa mwanamke wa kwanza nchini Israeli kuwa kamanda wa Brigedia, baada ya kupandishwa cheo na kuwa Kanali. Miongoni mwa waliompomgeza ni Waziri wa Uchumi, Orna Barbivai, Meja Jenerali wa kwanza wa kike Israeli pic.twitter.com/6eThLzPpU5
— ๐๐๐ฌ๐ฎ๐ฌ๐ข (@Chahali) June 18, 2022
#HabariNiMuhimuKulikoUbuyu: Mahakama ya rufani ya kijeshi nchini Tunisia imemhukumu mwanasiasa maarufu wa upinzani Seifeddine Makhlouf kifungo cha mwaka mmoja jela kwa kosa la kumtukana jaji. Hatua hiyo imetafsiriwa kuwa mwendelezo wa udikteta wa Rais Kais Saied (pichani) pic.twitter.com/eeK3oVptmK
— ๐๐๐ฌ๐ฎ๐ฌ๐ข (@Chahali) June 18, 2022
#HabariNiMuhimuKulikoUbuyu: Wimbi la changamoto za kiusalama zinazoikabili Naijeria linazidi kukua, ambapo kwa upande mmoja kumeubuka mapigano ya kikabila katika jimbo la Adamawa, na kwa upande mwingine wimbi la ubakaji dhidi ya watoto linaongezeka katika jimbo la Borno pic.twitter.com/lgIZMqTgxC
— ๐๐๐ฌ๐ฎ๐ฌ๐ข (@Chahali) June 17, 2022
#HabariNiMuhimuKulikoUbuyu: Rais wa Korea ya Kaskazini Kim Jong Un na mkewe Ri Sol Ju wametoa mchango wa "madawa kwa matumizi ya familia yao" kusaidia kukabili ugonjwa mpya wa matumbo katika mji wa kusini Haeju pic.twitter.com/YEZGlb6eTh
— ๐๐๐ฌ๐ฎ๐ฌ๐ข (@Chahali) June 17, 2022
#HabariNiMuhimuKulikoUbuyu : Wasanii Falz na Teni wa Naijeria wamesapoti kujiandikisha kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu nchini humo, kwa kufanya tamasha ambalo "kiingilio" kilikuwa kadi ya mpiga kura. Kadhalika, ukumbini kulikuwa na kituo cha kujiandikisha kupiga kura pic.twitter.com/PlPrD3O8gI
— ๐๐๐ฌ๐ฎ๐ฌ๐ข (@Chahali) June 16, 2022
#HabariNiMuhimuKulikoUbuyu: Kansela Olaf Scholz wa Ujerumani, Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa, na Waziri Mkuu Mario Draghi wa Italia wametembelea Ukraine kujionea wenyewe hali ilivyo nchini humo kufuatia uvamizi wa Urusi. pic.twitter.com/MK1aMeiHAv
— ๐๐๐ฌ๐ฎ๐ฌ๐ข (@Chahali) June 16, 2022
#HabariNiMuhimuKulikoUbuyu: Mapigano ya kikabila yanazidi kushamiri huko Darfur nchini Sudan ambapo hadi kufikia mwishoni mwa wiki iliyopita, jumla ya watu 49 wameuawa. Vijiji vinane vilichomwa moto katika siku za awali za mapigano hayo yaliyosababishwa na mgogoro wa ardhi. pic.twitter.com/aAvhOUyQ2J
— ๐๐๐ฌ๐ฎ๐ฌ๐ข (@Chahali) June 14, 2022
#HabariNiMuhimuKulikoUbuyu : Wanawake huko Ukanda wa Gaza sasa wanaweza kuripoti taarifa za unyanyasaji kupitia programu ya rununu iitwayo "Masahatuna" yaani "sehemu yetu." Programu hiyo ya rununu imetengenezwa na mhandisi wa kompyuta Alaa Huthut Ali pic.twitter.com/HQBG3B9TkF
— ๐๐๐ฌ๐ฎ๐ฌ๐ข (@Chahali) June 14, 2022
#HabariNiMuhimuKulikoUbuyu: Mataifa mawili yanayokabiliwa na vikwazo vya kimataifa, Irani na Venezuela, yamesaini makubaliano ya miaka 20 ya kushirikiana katika nyanja mbalimbali. Makubaliano hayo yamefikiwa wakati wa ziara ya Rais Maduro wa Venezuela nchini Irani pic.twitter.com/ebaflAz589
— ๐๐๐ฌ๐ฎ๐ฌ๐ข (@Chahali) June 11, 2022
#HabariNiMuhimuKulikoUbuyu: Waasi wa kundi la Nyatura wameua watu 7 katika kambi ya wakimbizi, Rujagati, mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Kwa mujibu wa taarifa, waasi hali walifanya mashambulizi Jumatano na Alhamisi wiki hii. pic.twitter.com/uS9xQLMip8
— ๐๐๐ฌ๐ฎ๐ฌ๐ข (@Chahali) June 11, 2022
#HabariNiMuhimuKulikoUbuyu: Mtandao wa kijamii wa TikTok umebainika kuwa unachochea usambazaji wa habari potofu na kuhamasisha ghasia za kisiasa kuhusiana na uchaguzi mkuu nchini Kenya utakaofanyika Agosti mwaka huu. Hayo yamebainishwa katika utafiti wa Taasisi ya Mozilla pic.twitter.com/cNcTkXAPRQ
— ๐๐๐ฌ๐ฎ๐ฌ๐ข (@Chahali) June 10, 2022