Categories
Habari

Sabaya Ahukumiwa Kifungo cha Miaka 30, Kukata Rufaa

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake watatu wamehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha.

Akitoa hukumu hiyo jana Oktoba 15, 2021 Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Arusha, Odira Amworo amesema ameridhika kuwa upande wa mashtaka umethibitisha mashtaka dhidi ya Sabaya na wenzake.

Agosti 24 mwaka huu, Sabaya na wenzake Sylvester Nyegu na Daniel Mbura walikamilisha kujitetea mahakamani hapo baada ya Jamhuri kukamilisha mashahidi 11 na vielelezo vinane.

Sabaya alifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Juni 4, mwaka huu baada ya kukamatwa Mei 27 wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya hukumu hiyo, Wakili wa Sabaya na wenzake Mosses Mahuna amesema hawajaridhika na hukumu hiyo iliyotolewa kwa sababu ina upungufu mwingi

SOURCE