Categories
Habari

NHC Yatelekeza Miradi Ya Mabilioni Chato

NAIBU Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk Angeline Mabula, amesikitishwa kwa kusuasua kwa utekelezaji wa miradi ya shirika la Nyumba la Taifa (NHC) wilayani Chato mkoani Geita.

Dk Mabula ambaye alitembelea na kukagua miradi hiyo leo Septemba 14, 2021 alionyesha kusikitishwa kutokana na kusuasua kwa utekelezaji wake kunakosababishwa na ucheleweshaji wa fedha.

Miradi mitatu inayotekelezwa na NHC ni mradi wa mnada wa mifugo Buzirayombo wenye thamani ya shilingi Bilioni 4.8, mradi wa ujenzi wa shule maalum ya Mbuye Bilioni 5.14 pamoja na mradi wa nyumba 20 za watumishi wa hospitali ya Rufaa ya Kanda- Chato wa thamani ya shilingi Bilioni 1.139

Akizungumza mara baada ya kukagua miradi yote mitatu Dk Mabula alisema, miradi hiyo ni muhimu na inapaswa kukamilika kwa wakati ili ianze kutumika.

Aidha Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa Mkoa wa Kagera, Maneno Mahenge, alimwambia Dk Mabula kuwa shirika lake la NHC limekuwa likisuasua kutekeleza kwa kasi miradi katika wilaya hiyo kutokana na kutopatiwa fedha za miradi kwa wakati.

CHANZO