Categories
Habari Kimataifa

Mtanzania Humprey Magwira, 20, Auawa kwa Risasi Houston, Marekani baada Ya Kusababisha Ajali Ndogo

Mtanzania Humphrey Maghwira ameuawa kwa kupigwa risasi huko Houston, jimbo la Texas, bchini Marekani baada ya kusababisha ajali ndogo, Ijumaa iliyopita.

Humprey mwenye umri wa miaka 20 alikuwa mwanafunzi wa mwaka wa pili katika fani ya uhandisi wa kompyuta, katika chuo kikuu cha Houston.

Marehemu aliyehamia Marekani akiwa na umri wa miaka 11, alifariki baada ya kufikishwa hospitali, kufuatia majeraha makubwa yaliyotokana na kupigwa risasi.

Mkazi mmoja wa Houston, Ramon Vasquez, mwenye umri wa miaka 19, amekamatwa Jumamosi asubuhi, na kufunguliwa mashtaka ya mauaji hayo.

Tulidhani ni wazo zuri kuja nchi hii kwa elimu bora kwa wanangu.

Exuperius Magwira, baba wa marehemu

Alikuwa mtoto mwema, mtoto mwema sana.

Josephine Kuyangana, mama wa marehemu

Wazazi hao walieleza kuwa ndoto zao njema kuhusu kijana wao zilivunjika usiku wa Ijumaa iliyopita baada ya polisi kuwafahamisha kuwa marehemu aligonga gari, na mwenye gari hilo alitoka garini na kummwagia risasi Humphrey.

Ni ngumu mno. Sijaweza kula chochote tangu mwanangu auwawe.Ni ngumu kwangu kula chochote. Ni ngumu kwangu kulala.

Exuperius Magwira