Categories
Habari

Monduli: Kundi La Wamasai Washambulia Gari La DC

Kundi la Masai katika kijiji Cha Moita wilayani Monduli wamevamia gari la mkuu wa wilaya hiyo ,Frank Mwaisumbe na kushambulia gari lake na kuvunja vioo wakati alipoenda kutuliza mgogoro wa ardhi uliokuwa unaendelea.

Mbali na uharibifu huo wananchi hao wakiwa na silaha za jadi waliamua kujichukulia sheria mkononi kwa kukatakata mabomba na matenki ya maji na Kisha baada ya uharibifu huo walibaini wametenda kosa na kuamua kukimbilia Makao makuu ya ccm Mkoani Arusha Kuficha madhambi yao

Hata hivyo Katibu mkuu wa CCM Mkoa wa Arusha,Musa Matoroka aliongea nao katika kikao cha ndani ofisini na baadaye walitoka nje huku Katibu huyo akisikika alisema tumemalizana nao.

Wakati wakiteremka nje ya Makao makuu ya ccm Ghafla gari la Polisi Kutoka wilayani Monduli ilifika na kufanikiwa kuwakamata baadhi Yao ambapo baadaye polisi waliwaachia .

Chanzo Cha vurugu hizo bado hakijafahamika ila taarifa za awali zinadai kwamba Kuna mtu amejimilikisha eneo kubwa la Ardhi kinyume na utaratibu na kusababisha wakose eneo la malisho