#HabariNiMuhimuKulikoUbuyu: Wakati serikali ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ikitangaza mnada wa vitalu vya mafuta, kuna wasiwasi kuwa zoezi hilo litaishia kuwanufaisha mafisadi wachache badala ya manufaa kwa taifa hilo masikini lakini linaloongoza kwa rushwa duniani pic.twitter.com/22lk6d3AAg
— 𝐉𝐚𝐬𝐮𝐬𝐢 (@Chahali) July 30, 2022
#HabariNiMuhimuKulikoUbuyu: kwa muda mrefu, changamoto dhidi ya ustawi wa wanyamapori imekuwa janga la ujangili. Hata hivyo, imeripotiwa kuwa nchini Kenya, mabadiliko ya tabianchi ndio tishio kubwa kwa uhai wa tembo kuliko ujangili. Zaidi ya tembo 20 wamekufa kutokana na ukame pic.twitter.com/c2s3it1lbn
— 𝐉𝐚𝐬𝐮𝐬𝐢 (@Chahali) July 30, 2022
#HabariNiMuhimuKulikoUbuyu: Vitendo vya ugaidi na ujambazi ambavyo vimekuwa vikiyumbisha usalama nchini Nigeria, vimetajwa kuathiri shughuli za kilimo huko Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo. Wakazi mbalimbali wa maeneo hayo wamekimbia makazi yao – na mashamba yao – pic.twitter.com/jQQZWCLEGg
— 𝐉𝐚𝐬𝐮𝐬𝐢 (@Chahali) July 25, 2022
#HabariNiMuhimuKulikoUbuyu: Utawala wa kijeshi nchini Myanmar umewanyonga wabunge wa zamani watatu, na wafungwa wa kisiasa watatu, licha ya wito kutoka sehemu mbalimbali duniani kuutaka utawala huo wa kidikteta usifanye hivyo pic.twitter.com/2dEleye6q5
— 𝐉𝐚𝐬𝐮𝐬𝐢 (@Chahali) July 25, 2022
#HabariNiMuhimuKulikoUbuyu: Waziri Mkuu wa Italia, Mario Draghi amejiuzulu kufuatia wenza wanaounda serikali ya mseto kugoma kumuunga mkono. Kufuatia hatua hiyo, kutakuwa na uchaguzi hivi karibuni ambapo mwanasiasa mwenye mrengo mkali wa kulia Giorgia Meloni anatarajiwa kushinda pic.twitter.com/MQeIsCbec4
— 𝐉𝐚𝐬𝐮𝐬𝐢 (@Chahali) July 21, 2022
#HabariNiMuhimuKulikoUbuyu: Rais Joe Biden wa Marekani amekutwa na maambukizi ya UVIKO-19. Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 79 alishapata chanjo dhidi ya maambukizi ya ugonjwa huo, anaendelea vema na wasaidizi wake wameeleza kuwa anaendelea na majukumu yake ya kazi pic.twitter.com/loOBxRUdCG
— 𝐉𝐚𝐬𝐮𝐬𝐢 (@Chahali) July 21, 2022
#HabariNiMuhimuKulikoUbuyu Rais Paul Kagame wa Rwanda amewapandisha vyeo mabrigedia watatu wa jeshi la nchi hiyo kuwa mameja jenerali. Waliopandishwa vyeo ni brigedia Vincent Nyakarundi, Willy Rwagasana na Ruki Karusisi. Pia kanali Ronald Rwivanga amepandishwa cheo kuwa Brigedia pic.twitter.com/MOXC29ewEU
— 𝐉𝐚𝐬𝐮𝐬𝐢 (@Chahali) July 16, 2022
#HabariNiMuhimuKulikoUbuyu Rais Yoweri Museveni wa Uganda amemshauri Rais Felix Tshisekedi wa DRC kufanya mazungumzo na waasi wa kundi la M23 ili kumaliza mapingano yanayoendelea. Rais Museveni alitoa rai hiyo alipokutana na msafara ulioleta ujumbe kutoka DRC (pichani) pic.twitter.com/M68kv1TDvJ
— 𝐉𝐚𝐬𝐮𝐬𝐢 (@Chahali) July 16, 2022
#HabariNiMuhimuKulikoUbuyu: Rais Sergio Mattarella wa Italia amekataa ombi la Waziri Mkuu wa nchi hiyo Mario Draghi (pichani) aliyetaka kujiuzulu kufuatia kuyumba kwa mshikamano ndani ya vyama vinavyounda serikali ya mseto ya nchi hiyo. pic.twitter.com/M55BAUa5ql
— 𝐉𝐚𝐬𝐮𝐬𝐢 (@Chahali) July 15, 2022
#HabariNiMuhimuKulikoUbuyu: Hatimaye Rais Gotabaya Rajapaska wa Sri Lanka ametangaza kujiuzulu rasmi. Ametuma baruapepe akiwa Singapore alikokimbilia kufuatia wimbi la maandamano ya wananchi waliokuwa wakilalamikia uongozi wake mbovu katika uchumi. pic.twitter.com/9JyaPtYDLO
— 𝐉𝐚𝐬𝐮𝐬𝐢 (@Chahali) July 15, 2022
#HabariNiMuhimuKulikoUbuyu: Kiongozi wa utawala wa kijeshi nchini Sudan, Jenerali Abdel-Fatah al-Burhan amewateua majenerali wa zamani watano kuwa mabalozi katika nchi jirani. Uteuzi huo umetafsiriwa kuwa ni mbinu ya mtawala huyo kuimarisha nguvu zake ndani na nje ya nchi hiyo pic.twitter.com/aUMeNyl2av
— 𝐉𝐚𝐬𝐮𝐬𝐢 (@Chahali) July 12, 2022
#HabariNiMuhimuKulikoUbuyu: Marekani inadai kwamba Urusi imetuma maombi kwa Irani ipatiwe ndege ndogo zisizo na rubani (drones) ili zitumike kwenye uvamizi huko Ukraine. Hata hivyo, haijafahamika endapo Urusi imeshaanza kupokea ndege hizo pic.twitter.com/nAsVpKtDkf
— 𝐉𝐚𝐬𝐮𝐬𝐢 (@Chahali) July 12, 2022