Categories
Habari

Mama @SuluhuSamia Acharuka, Avunja Bodi ya TPA na Wakala wa Meli, Aagiza Waliotajwa Ripoti ya CAG Kuchukuliwa Hatua Haraka

Mkurugenzi wa TPA, Waziri na TAKUKURU mpo, naamrisha ripoti ya CAG mkaisome, halafu mchukue hatua, fedha nyingi sana imepotea watu tunachekeana tu, na bado waliotajwa kwenye ripoti bado wapo maofisini wanaendeleza wizi,

Ripoti ya CAG inasema kwamba kulikuwa na malipo ya juu ya wakandarasi bila kufuata sheria za manunuzi na matumizi, ilitaja pia watu waliohusika na ubadhirifu na kupendekeza hatua za kuchukuliwa ambazo hazikuchukuliwa hadi leo

Kuna makundi wanajua wanayoyafanya ndani ya serikali, na yanageuka kusema serikali ya awamu ya 6 ufisadi umerudi mambo yako hovyo kumbe wao ndio wako hovyo, mambo hayo yalifanyika huko nyuma, gari bovu linaangushiwa awamu ya 6 sitakubali