Categories
Habari

Mama Samia Mgeni Rasmi Mkutano wa Vyama vya Siasa Desemba 16 hadi 17

Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mkutano wa vyama vya siasa pamoja na wadau mbalimbali wa siasa

Mkutano huo ambao awali ulitakiwa kufanyika Oktoba 21, mwaka huu lakini ukahairishwa, imeelezwa kuwa utafanyika Desemba 16 na 17, mwaka huu jijini Dodoma.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumamosi Desemba 4, 2021 Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya siasa, Juma Ally Khatib amesema mkutano huo utatanguliwa na semina kwa wajumbe wa baraza la vyama vya siasa kuhusu historia na majukumu ya baraza hilo, ambayo itafanyika Desemba 15.

Khatib amebainisha kuwa mkutano huo utakuwa na mada tatu zinazohusu masuala ya kisheria, demokrasia, siasa, uchumi na maadili ya kitaifa, yanayohusiana na demokrasia ya vyama vingi vya siasa.

“Baraza la vyama vya Siasa linatumia fursa hii, kushauri vyama vya siasa vyote vyenye usajili kamili, kuhudhuria mkutano huo, kwani ni fursa adhimu ya kubadiishana mawazo kuhusu mambo yanayotuhusu. Siasa ni ushawishi na ushawishi hufanikiwa kapitia njia ya mijadiliano,” amesema Khatib.