Categories
Habari

Makamu Rais Wa #MissEastAfrica2021 @JollyMutesi Ampongeza Mama @SuluhuSamia Kwa Hamasa Anayowapa Wasichana

Makamu wa Rais wa waandaaji wa mashindano ya kumsaka mlimbwende wa Afrika Mashariki kwa mwaka huu 2021, Miss Rwanda wa mwaka 2016, Jolly Mutesi, ametoa pongezi kwa Rais wa sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu, hususan kwa kuwa hamasa kwa wanawake na wasichana.

Tamko kamili la Jolly kama lilivyotafsiriwa kwa Kiswahili

Ningependa kuungana na kaka zangu na dada zangu wa Tanzania kumpongeza Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, kwa kuwa Raia mwanamke wa kwanza Afrika Mashariki. Inawakumbusha wanawake wote barani Afrika kwamba wanawake ni wanadamu wenye uwezo mkubwa na hakuna cha kuwazuwia pindi wakipewa nafasi. Wewe (Mama Samia) ni kioo halisi cha mwanga na nguvu ya mwanamke, na kwa hakika hakuna taifa linaloweza kupiga hatua bila mchango wa mwanamke. Tunajivunia nafasi yako na asante kwa kuwa hamasa kwa wasichana wengi.