Categories
Habari

Dear Mama Samia, Bandari Ya Dar Imeuzwa? Zambia Yalalamikiwa Kwa Kujimilikisha Kazi Ya Kubeba Mizigo Bandarini Hapo

Chama cha Wamiliki Malori Tanzania(TATOA) Wameiomba Serikali kuingilia kati Sheria iliyotungwa Zambia ya kusimamia Uingiaji na utokaji wa Mizigo Nchini Zambia.

Sheria hiyo inataka Mizigo yote inayoingia Zambia, 50% ibebwe na Wazambia Wazawa, 30% ibebwe na TAZARA na 20% ibebwe na Watu wengine.

Akiongea na Wanahabari, leo 24June 2021 Mkoani Dar Es Salaam, Makamu Mwenyekiti wa Tanzania Truck Owners Association( TATOA) TATOA ndugu ELIAS Lukumay amesema kitendo hicho ni kinyume na muongozo wa SADC ambao unaelezea kuwe na biashara Huria, na inataka tushindane kwa ubora na bei si Sheria kandamizi.

Lukumay amesema, hili tatizo lisipofanyiwa kazi, Malengo ya Tanzania ya Kupitisha Mizigo Bandari ya Dar Es Sakaam ya kufikia Tani Milioni 30 kwa Mwaka haitafikiwa. Sasa hivi Tanzania inapitisha Mzigo tani Milioni 17 kwa Mwaka.

Amesema Tanzania inaboresha Miundombinu ya bandari na barabara. Lakini hatua hii ya Zambia itafanya Watanzania Wasinufaike na Bandari ya Dar Es Salaam. Pia Wasafirishaji wa Tanzania wamekopa kwenye Mabenki Mbalimbali, hivyo hii Sheria kama itatekelezwa Zambia, itapelekea Kampuni nyingi za Tanzania kufilisika.

Wamemuomba rais Samia awasaidie kuondoa hii kero kwani Watanzania hawataruhusiwa Magari yao Kupeleka Mizigo Zambia

Amechukua nafasi hiyo ya kuongea na Wanahabari kumpongeza kwa jinsi alivyoongeza Ufanisi wa Utendaji Bandarini. Foleni ya Malori imeisha, Utendaji umekuwa mzuri.