App ya Telegram inayosifika kama moja ya apps salama zaidi kwa mawasiliano ya faragha kwa watumiaji, imezindua uwezo wa kupiga simu za video (video calls).

Uzuri katika hatua hii ni kwamba maongezi kwa njia ya video yatafanyika huku yakilindwa na usimbaji fiche (encryption). Maana yake ni kwamba mawasiliano hayo yatakuwa salama na kukwepa mamlaka za serikali kusikiliza maongezi

Kwa sasa, mawasiliano kwa video ni kwa kati ya mtu na mtu tu lakini baadaye itawezekana kwa kundi la watu kufanya mawasiliano kwa pamoja (group video calls).