
Category: Siasa



Moja ya habari zilizovuma kwenye vyombo vya habari vya Marekani ni mahojiano kati ya rapa maarufu wa kike wa Marekani, Cardi B na mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Democrats, Joe Biden. Kwa vile Tanzania nayo inajiandaa na kinyang’anyiro cha uchaguzi kama ilivyo Marekani, mahojiano hayo yanaweza kuwa funzo nzuri kwa wasanii mbalimbali nchini […]

Uchaguzi Mkuu wa unaotarajiwa kufanyika hapo Oktoba umeendelea kutawaliwa na vitimbi baada ya kupatikana taarifa kuwa mgombea hewa, kada ya CCM, amechukua fomu ya kugombea ubunge jimbo la Ubungo jijini Dar kwa tiketi ya Chadema. Taarifa iliyotolewa na aliyekuwa Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniphace Jacob, inamtaja mgombea huyo hewa kuwa ni Athumani Abdalla Sudi.


Ratiba za chama tawala CCM zinaonesha kuwa vikao vya Kamati Kuu wa CCM vilipaswa kufanyika Agosti 7 na 8 lakini hadi leo, takriban wiki sasa, hakuna kikao kilichoketi. Ajenda kuu ya kikao hicho ni kupitisha majina ya Wagombea wa Ubunge wa Majimbo wa CCM Tanzania Bara na Visiwani. Kwa mujibu wa taarifa, sababu kuu iliyopelekea […]

Aidha amewataka wanachama, wafuasi na wapenzi wa CHADEMA kuhakikisha kuwa wanawasindikiza wagombea wao wa Udiwani na Ubunge wanapokwenda kuchukua fomu za kuomba uteuzi ktk ofisi za DEDs ama TCDs ama CCDs ama WEOs ambao ndiyo wanaoratibu mchakato wa uchaguzi kwa niaba ya Tume ya Uchaguzi wa Taifa (NEC) katika ngazi ya Jimbo na Kata. Vivyo […]

Kwa mujibu wa taarifa, kituo cha runinga cha Azam kiliweka bandiko kwenye ukurasa wake katika mtandao wa kijamii wa Instagram, kisha ikafuta bandiko hilo. Hata hivyo baadhi ya wananchi walibahatika kuona bandiko hilo kabla halijafutwa. Maelekezo Kutoka Juu au Uoga Tu? Swali miongoni mwa wananchi wengi ni endapo kitendo hicho cha chombo hicho cha habari […]