Tamko hilo la Zitto ni kama kupigia mstari kauli hii ya Maalim Seif Sharif Hamad Macho na masikio sasa yaelekezwa kwa Bernard Membe, kada wa zamani wa CCM aliyefukuzwa na chama hicho tawala kisha akajiunga na ACT-Wazalendo, kabla ya kupitishwa kuwa mgombea wa chama hicho katika nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. […]
