Categories
Biashara

Erick Kabendera:Ushahidi Wa Matukio Yote Ya Vitisho Ninao Katika Picha Za Video

Huenda tarehe 24 Februari, 2020 ndio ilikuwa siku ya furaha zaidi kwa mwandishi wa habari za kiuchunguzi Tanzania, Erick Kabendera.

Aliachiwa huru baada ya kukaa gerezani kwa miezi saba nchini humo. Mashtaka yaliokuwa yamemkabili ni pamoja na uhujumu uchumi, kujihusisha na genge la uhalifu na ukwepaji wa kulipa kodi.

Anafahamika kwa kuandikia magazeti mbalimbali ya Kimataifa kama vile The Guardian na The Times ya Uingereza na pia magazeti ya nchini Tanzania.

Hii ni mara yake ya kwanza kuzungumza na chombo chochote cha habari. Mwandishi wa BBC Zuhura Yunus amemhoji akiwa mjini London, katika sehemu ya Kwanza ya mahojiano, Kwanza akitaka kujua yaliojiri siku aliyokamatwa

Chanzo: BBC Swahili