Categories
Biashara Habari

Biashara Ya Uume Wa Ng’ombe Yapamba Moto 😊

Dar es Salaam. Ukistaajabu ya Mussa utayaona ya Firauni! Msemo huu unajidhihirisha baada ya kauli ya Onesmo Mbasha, ambaye ni mmoja wa vijana wanaouza bidhaa mbalimbali zitokanazo na wanyama zikiwamo sehemu za uzazi za ng’ombe dume zinazojumuisha uume na korodani.

Zipo taarifa kuwa viungo hivyo vya ng’ombe ni maalumu kwa ajili ya kutengenezea nyuzi zinazotumika kuwashonea watu waliopata ajali na chakula kinachotumika zaidi nchini China.

Daktari wa mifugo kutoka The Old Farm House, Wilfred Hongoli anasema uume wa ng’ombe unaweza kutumika kutengenezea nyuzi za kushonea binadamu au mnyama pale anapopata majeraha au kufanyiwa upasuaji.

“Nyuzi zinazotengenezwa na bidhaa hiyo huwa na tabia ya kubaki mwilini hata baada ya jeraha kupona, tofauti na nyingine ambazo lazima zitolewe baada ya jeraha kupona,” alisema.

Hata hivyo, Onesmo anasema kabla ya kuanza biashara hiyo alikuwa na biashara ya nguo alizokuwa akizitoa Mombasa nchini Kenya na kuziuza katika Soko la Kariakoo.

Chanzo: Mwananchi