
Licha ya kauli ya mmiliki wa mtandao wa kijamii wa Twita, Elon Musk, aliyoitoa jana kwamba ataondoa “block button”, ukweli ni kwamba hawezi kufanya hivyo.
Sheria za Google Play na Apple Store, sehemu mbili ambazo bila uwepo wake, Twitter itashindwa kufanya kazi kwa ufanisi, zinataka kila app kuwa na nyenzo ya kumwezesha mtumiaji wa app hiyo kubloku wasumbufu wa mtandaoni.
