Categories
Safu ya Maisha

Mfululizo wa makala zinazofundisha jinsi ya kutumia “48 Laws of Power” katika maisha yako ya kila siku: Sehemu ya Kwanza – Orodha ya Laws zote na tafsiri yake kwa Kiswahili

Tafsiri ya moja kwa moja ya 48 Laws of Power sio rahisi sana kwa sababu ya muktadha wa neno power. Lakini kwa minajili ya makala hizi, neno hilo linamaanisha zaidi mamlaka au/na nguvu. Kwahiyo, kwa Kiswahili, 48 Laws of Power inaweza kutafsiriwa kuwa “Kanuni 48 za Mamlaka/Nguvu.”

Baada ya utangulizi huo, sasa twende kwenye kitabu husika. Hiki ni moja ya vitabu bora kabisa katika suala zima la Jinsi Ya Kuwa Mtu Bora (tafsiri isiyo rasmi ya Personal Development).

Kwa kifupi kabisa, mantiki ya kitabu hiki ni hii: tunaishi katika dunia iliyosheheni watu makatili, wenye roho mbaya, wasio na huruma, wachokozi, wenye wivu, wenye kisasi, washirikina, wabinafsi, wanaofurahi matatizo ya wenzao, wanaokandamiza wenzao, wanaotesa, wanyanyasaji…kwa kifupi, dunia haina uhaba wa watu wabaya.

Na kitabu hiki kinakupa mikakati ya kusalimika katika dunia iliyosheheni watu hao.

Ili kuepuka mkanganyiko wa tafsiri, kocha wako atatumia neno law badala ya tafsiri ya Kiswahili ya neno hilo ya sheria, kanuni,nk.

Mpangilio ni kwamba kocha wako atakuletea laws moja hadi mbili kwa wiki na kuzifafanua kwa kina.

Lakini kabla ya yote, hizi hapa laws zenyewe kwa Kiingereza na tafsiri yake kwa Kiswahili kwenye mabano

 1. Never outshine the master. [Usitake kumpiku bosi wako. Neno ‘bosi’ hapa linatumika kumaanisha mtu mwenye mamlaka zaidi yako, na sio lazima katika mazingira ya kazi pekee]
 2. Never put too much trust in friends; learn how to use enemies. [Usiweke imani kubwa sana kwa marafiki; jifunze jinsi ya kuwatumia maadui]
 3. Conceal your intentions. [Ficha ni yako]
 4. Always say less than necessary. [Wakati wote, usiseme zaidi ya kile unachopaswa kusema]
 5. So Much Depends on Reputation. Guard it with your Life. [Vitu vingi vinategemea hadhi yako. Ilinde kwa nguvu zako zote]
 6. Court attention at all costs. [Nasa mvuto wa watu kwako, kwa gharama yoyote ile. Neno mvuto hapa linamaanisha ile hali ya watu kuchukua muda wao au kuacha shughuli zao, na kukupa muda wao kukusikiliza, kukusoma,kukuona,nk]
 7. Get others to do the work for you, but always take the credit. [Wafanye watu watende jukumu kwa ajili yako, lakini mara zote wewe ndio uchukue sifa kutokana na matokeo chanya ya jukumu hilo]
 8. Make other people come to you; use bait if necessary. [Fanya watu waje kwako – kwa mfano kuhitaji msaada,ushauri,nk – tumia chambo kama itahitajika]
 9. Win through your actions, never through argument. [Shinda kwa vitendo, kamwe si kwa malumbano]
 10. Infection: avoid the unhappy and unlucky. [Maambukizi: epuka watu wasio na furaha na wenye mikosi]
 11. Learn to keep people dependent on you. [Jifunze kuwafanya watu wakutegemee]
 12. Use selective honesty and generosity to disarm your victim. [Tumia ukweli na wema wa kimkakati kumuondolea uwezo wa kujikinga mtu unayemlenga]
 13. When asking for help, appeal to people’s self-interests, never to their mercy or gratitude. [Unapoomba msaada, vutia maslahi yao, kamwe isiwe kutokana na huruma yao au wema wao]
 14. Pose as a friend, work as a spy. [Jiegeshe kama rafiki, fanya kazi kama jasusi
 15. Crush your enemy totally. [Mwangamize kabisa adui yako]
 16. Use absence to increase respect and honor. [Adimika ili kuongeza heshima]
 17. Keep others in suspended terror: cultivate an air of unpredictability.[Wafanye watu wawe kwenye hofu iliyoahirishwa, tengeneza hali ya ya kutotabirika]
 18. Do not build fortresses to protect yourself. Isolation is dangerous. [Usijenge ngome kujilinda. Kujitenga ni hatari]
 19. Know who you’re dealing with; do not offend the wrong person. [Elewa unadili na mtu gani; kamwe usimtibue mtu asiyestahili kutibuliwa]
 20. Do not commit to anyone. [Usijifunge kwa mtu yeyote ule]
 21. Play a sucker to catch a sucker: play dumber than your mark. [Jifanye zuzu kumnasa zuzu: onekana mjinga kuliko uwezo wako ulivyo]
 22. Use surrender tactic: transform weakness into power [Tumia mbinu ya kujisalimisha: fanya udhaifu kuwa nguvu]
 23. Concentrate your forces. [Imarisha ‘majeshi’ yako]
 24. Play the perfect courtier. [Jifanye mhudumu mtimilifu]
 25. Re-create yourself. [Jitengeneze upya mwenyewe]
 26. Keep your hands clean. [Usijichafue – sio na uchafu wa taka bali kutojihusisha na mambo yanayoweza kuharibu taswira au hadhi yako]
 27. Play on people’s need to believe to create a cult-likefollowing. [Tumia mahitaji ya watu kutengeneza wafuasi watiifu]
 28. Enter action with boldness. [Ingia shughulini kwa ushupavu]
 29. Plan all the way to the end. [Panga jambo hatua kwa hatua hadi mwisho wake]
 30. Make your accomplishments seem effortless. [Fanya mafanikio yaonekane kuwa yalipatikana bila jitihada kubwa]
 31. Control the options: get others to play with the cards you deal. [Miliki hiari; wafanye watu wafanye mambo kutokana na matakwa yako]
 32. Play to people’s fantasies. [Tumia tamaa za watu kutimiza matakwa yako]
 33. Discover each man’s thumbscrew. [Fukua makaburi – kwa maana ya kuchimba mapungufu, siri, mabaya, aibu, nk kuhusiana na mlengwa]
 34. Be royal in your fashion: act like a king to be treated like one. [Fanya mambo yako kifalme: ili uheshimiwe kama mfalme, tenda mambo yako kama mfalme]
 35. Master the art of timing. [Kuwa mbobezi kwenye sanaa ya mpangilio wa muda]
 36. Disdain things you cannot have: Ignoring them is the best revenge. [Tweza vitu ambavyo huwezi kuwa navyo: kuvipuuza ni kisasi stahili]
 37. Create compelling spectacles. [Tengeneza matukio ya kuvutia hisia za watu]
 38. Think as you like but behave like others. [Waza utakavyo lakini tenda kama wengine]
 39. Stir up waters to catch fish. [Tikisa maji kukamata samaki]
 40. Despise the free lunch. [Tweza vitu vya bure]
 41. Avoid stepping into a great man’s shoes. [Epuka kuvaa viatu vya mtu mahiri. Hapa neno kuvaa viatu linamaanisha kushika nafasi ya mhusika]
 42. Strike the shepherd and the sheep will scatter. [Mtandike mchunga mifugo, na mifugo itasambaa]
 43. Work on the hearts and minds of others. [Jitahidi kugusa akili na nyoyo za watu wengine]
 44. Disarm and infuriate with the mirror effect. [Inyanganye nguvu na kuigadhabisha tabia inayomwezesha mtu kuiga nafsi au/na matendo yako]
 45. Preach the need for change, but never reform too much at once. [Hubiri umuhimu wa mabadiliko, lakini kamwe usilete mageuzi kwa mkupuo]
 46. Never appear perfect. [Kamwe usionekane mtimilifu]
 47. Do not go past the mark you aimed for; in victory, learn when to stop. [Usivuke hatua uliyoikusudia; katika ushindi, jifunze jinsi ya kuhitimisha]
 48. Assume formlessness. [Kuwa mtu usiyeelezeka, usiyeshikika]

Itaendelea kwenye toleo la wiki ijayo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *