Categories
Habari za Uchumi na Biashara

Suala la mikopo ya nje lililomng’oa Ndugai laibuka tena

Rais Samia Suluhu ameanza ziara ya siku 6 nchini Korea ya Kusini.

Moja ya yanayotajwa kuwa mafanikio ya ziara hiyo ni kusainiwa kwa mkopo wenye masharti nafuu ambapo Korea ya Kusini itaikopesha Tanzania shilingi trilioni 6.51.

Hata hivyo, habari ya mkopo huo imerejesha mjadala uliopelekea Spika wa zamani wa Bunge la Muungano, Job Ndugai, ajiuzulu baada ya kutahadharisha kuwa “kuna siku nchi itauzwa” kutokana na wimbi la mikopo ya nje.

Baadhi ya wananchi kwenye mitandao ya kijamm walikumbushia onyo hilo la Ndugai kuhusu mikopo.

Kadhalika wengine walidai kwamba “kukopa harusi kulipa matanga”wakimaanisha kuwa Watanzania watakamuliwa huko mbeleni ili kumudu kulipa madeni hayo.

Pia baadhi walonyesha hofu kuwa mikopo hiyo inaishia kuwanufaisha zaidi mafisadi

Hata hivyo watetezi wa mikopo wadai kuwa sio suala la ajabu kwa Tanzania kukopa kwani kila nchi duniani hukopa.

Vilevile, walieleza kuwa suala sio kukopa bali mikopo hiyo inaelekezwa kwenye sekta gani. Walisema kuwa wanaamini mikopo sio tu ni habari njema kwa Tanzania na Watanzania bali pia inaonyesha kuwa Tanzania ipo vema kiuchumi ndio maana inakopesheka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *