Kufuatia mjadala uliojitokeza jana baada ya Bodi ya Wakurugenzi wa klabu ya Simba ya Tanzania kutangaza kuwa imemteua Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, Barbara Gonzalez, kuwa Afisa Mtendaji Mkuu kamili, gazeti la Habari Tanzania lilifanya mawasiliano na wataalamu wa masuala ya raslimali watu (human resources) na uajiri ili kupata mtazamo wao wa kitaalamu. […]
