Categories
Habari

Baadhi ya wakazi wa Manispaa ya Tanga walalamikia “maji yenye ladha ya chumvi.”

Baadhi ya wakazi wa Manispaa ya Tanga walioongea na “Habari Tanzania” wameeleza kuwa wanakabiliwa na tatizo la maji ya bomba yenye ladha ya chumvi. Kwa mujibu wa maelezo yao, tatizo hilo limedumu kwa takriban miezi mitatu sasa. Katika kukabiliana nalo, wakazi hao wamelazimika kuchemsha maji ya kunywa japo hata kufanya hivyo hakujaweza kutatua tatizo hilo.