Categories
Habari Siasa

Wabunge Wa ACT-Wazalendo Waapishwa, Wasema Hawatokwenda Nje Ya Nchi Kulalamika Masuala Ya Tanzania

Mbunge wa Jimbo la Konde kwa tiketi ya ACT-Wazalendo, Khatibu Said Hajj amesema masuala ya Tanzania yatazungumzwa Tanzania na sio nje ya nchi

Ameyasema hayo katia hafla ya uapisho wa wabunge wanne wa Zanzibar ambapo pia ametoa shukrani kwa Rais Hussein Mwinyi na Maalim Seif Hamad

Amesema maamuzi yaliyofanywa na viongozi wa juu wa ACT-Wazalendo yalikuwa ni kwa maslahi mapana ya Wazanzibar na wale wanaokebehi mapatano yao wataona aibu kwa kebehi zao

Amesema maridhiano yanapaswa kuungwa mkono na kila mtandania badala ya kudharau mapatano hayo. Na mambo ya Zanzibar ni watanzania wote, aidha wamesahau yote yaliyotokea na kusamehe