Categories
Habari Siasa

Wabunge 75 wa CCM “watupwa nje”

WABUNGE takribani 75 kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambao walijitosa kutetea nafasi zao katika uchaguzi mkuu wa 28 Oktoba mwaka huu, wameangukia pua.

Mkutano wa Halmashauri Kuu ya taifa (NEC), uliopitisha majina ya wagombea hao, ulifanyika jana Alhamisi, tarehe 20 Agosti 2020 chini ya mwenyekiti wake, Dk. John Magufuli.

Kati ya wabunge hao, yumo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe; Naibu Waziri wa Kilimo, Omar Mgumba na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dk. Mary Mwanjelwa.

Taarifa zinasema, katika orodha ya wabunge 264 -kwa maana ya majimbo 214 (Bara) na 50 ya Zanzibar – wamo wabunge wakongwe na maarufu, “waliokatwa.”

Mathalani, aliyepata kuwa mwanasheria mkuu wa serikali, waziri wa miundombinu na mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge, pamoja na kwamba alishinda kura za maoni katika jimbo lake la Bariadi Mashariki, lakini hakuteuliwa.

Wengine, ni mbunge wa miaka mingi na waziri wa zamani wa nishati na madini, William Ngeleja (Sengerema); aliyekuwa mbunge wa Kigoma Kaskazini, Peter Serukamba na aliyekuwa mbunge wa Busega, Raphael Chegeni.

Katika orodha hiyo, kuna wabunge wa viti maalum walioshindwa kura za maoni kwenye majimbo, akiwamo Angella Kairuki (Same Mashariki); Vick Kamata, aliyekuwa anataka kuligomboa jimbo la Kibamba na Halima Bulembo.

Wengine walioshindwa kupenya, ni Charles Tizeba (Buchosa), Balozi Adad Rajab (Muheza), Balozi Diodorus Kamala (Nkenge),Stephen Masele (Shinyanga Mjini), Julius Kalanga (Monduli), Maulid Mtulia (Kinondoni), Lolesia Bukwimba (Busanda), Juma Nkamia (Chemba), Chacha Ryoba (Serengeti) na Albert Obama (Buhigwe).

Wengine, ni Daniel Nsanzugwanko (Kasulu Mjini), Mbaraka Bawazir (Kilosa), Goodluck Mlinga (Ulanga), Suleiman Ahmed Saddiq (Mvomero), Abadallah Mtolea (Temeke), Haroon Pirmohamed (Mbarali), Rafael Gashaza (Ngara), Prof. Jumanne Maghembe (Mwanga), Hassan Masala (Nachingwea), Jitu Soni (Babati Vijijini) na Isaay Paulo (Mbulu Mjini).

Wamo pia, James Ole Millya (Simanjiro), Emmanuel Papian (Kiteto), Omar Badwel (Bahi), Issa Mangungu (Mbagala), Augustino Masele (Mbogwe), Venance Mwamoto (Kilolo), Godfrey Mgimwa (Kalenga), Mahmoud Mgimwa (Mufundi Kaskazini), Edwin Sannda (Kondoa Mjini) na Charles Kitwanga (Misungwi).

Wengine, ni Oscar Mukasa (Biharamulo Magharibi), Dk. Pundenciana Kikwembe (Kavuu), Richard Mbogo (Nsimbo), Christopher Chiza (Buyungu), Peter Serukamba (Kigoma Kaskazini), Prof. Noman Sigalla (Makete), Kangi Lugola (Mwibara), Deogratias Ngalawa (Ludewa), Hassan Kaunje (Lindi Mjini) na William Dau (Nanyumbu).

Wengine, ni Dk. Mary Nangu (Hanang), Hasna Mwilima (Kigoma Kusini), George Lubeleje (Mpwapwa), Joel Mwaka (Chinolwa) sasa Chamwino; Jerome Bwanausu (Lulindi), Rashid Chuachua (Masasi), Saul Amon (Rungwe), Peter Lijualikali (Kilombero), Nimrod Mkono (Butiama) na Victor Mwambalaswa (Lupa).

Katika orodha hiyo, wapo pia Dk. Shukuru Kawambwa (Bagamoyo), Dk. Haji Mponda (Malinyi), Omary Kigoda (Handeni Mjini), Mary Chatanda (Korogwe Mjini), Mboni Mhita (Handeni Vijijini), Edward Mwalongo (Njombe Mjini), Joram Hongoli (Lupembe), Greyson Lwenge (Wanging’ombe), Dk. Dalaly Kafumu (Igunga), Mussa Ntimizi (Igalula) na Ezekiel Maige (Msalala).

Wengine, ni Allan Kiula (Iramba Mashariki), Justin Monko (Singida Kaskazini), Janet Mbene (Ileje), John Kadutu (Ulyankulu) na Prof. Anna Tibaijuka (Muleba Kusini) , Salum Khamis (Meatu) na Daniel Mtuka (Manyoni Mashariki), Salum Khamis (Meatu) na Daniel Mtuka (Manyoni Mashariki).

Kupatikana kwa taarifa kuwa robo ya wabunge wa CCM wameenguliwa na chama chao; na au wamelazimishwa na wajumbe kustaafu, kunatokana na hatua ya NEC ya chama hicho, kuwapigia mstari mwekundu.