Categories
Habari Siasa

Ubunge Mwibara Kwa Tiketi Ya CCM: Kamati Kuu Yamkata “Mwanaharakati Huru” Musiba

Katibu Mwenezi wa CCM, Humprey Polepole ametangaza uamuzi wa Kamati Kuu ya chama hicho kuhusu majina ya wagombea nafasi za ubunge katika baadhi ya majimbo.

Moja ya majimbo yaliyovuta hisia za wengi ni Mwibara ambako mmoja wa wafuasi wakubwa wa Rais Magufuli, “mwanaharakati huru” Cyprian Musiba, alikuwa akiwania kupitishwa kugombea ubunge kwenye jimbo la Mwibara.

Hata hivyo, ndoto za ubunge za Musiba zimefikia ukingoni baada ya Polepole kutangaza kuwa mwana-CCM aliyepitishwa na Kamati Kuu ni Charles Kajege.

Taarifa hizo ni mbaya pia kwa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola, ambaye licha ya kuwa mbunge aliyemaliza muda wake, pia alishika nafasi ya kwanza kwenye kura za maoni.