Categories
Habari Siasa

Tundu Lissu: Naishi Kwenye Makazi Ya Balozi Wa Ujerumani Kwa Sababu Maisha Yangu Hayako Salama, Nitarejea Ubelgiji

Tundu Lissu akihojiwa na redio Ujerumani DW anasema amepata simu za kutishiwa amani na ameamua kujificha kwenye makazi ya Balozi wa Ujerumani

Anasema maisha yake yako hatarini na anajipanga kuondoka na kurudi Ubeligiji

Tundu ni mwanasheria na very treak man tujihadhari naye sana

=========

LISSU: Niko katika makazi ya balozi wa Ujerumani, Dar es Salaam tangu siku ya Jumatatu.

MWANDISHI: Kulikoni?
LISSU: Naishi kwenye makazi ya balozi kwa sababu maisha yangu hayako salama tangu siku ya Jumamosi iliyopita, napata ujumbe wa kunitishia maisha kwa hiyo niliondoka nyumbani kwangu siku ya Jumapili na siku ya Jumatatu nikaenda ubalozini, nikafatwa na askari polisi wa Tanzania wakiwa kwenye magari mawili, nikakamatwa nikapelekwa kituo cha polisi Central na isingekuwa uwepo wa maafisa wa kibalozi wa Ujerumani siku hiyo pengine nisingerudi nyumbani kwangu.

MWANDISHI(LILIAN MTONO): Unasema kwamba ulianza kupata vitisho siku ya Jumamosi kabla hujahamia kwenye makazi ya balozi, ni vitisho vya aina gani ulivipata na nani hasa alikuwa anakutisha?
LISSU: Siku ya Jumamosi nilipigiwa simu na mtu ambae hakujitambulisha akaniambia kwamba, mheshimiwa maagizo tuliyopewa ni kumalizana na wewe, once and for all na baadae kidogo nikaletewa simu nyingine na mtu mwingine aliniambia hivyo hivyo kwamba mheshimiwa oda ya kukumaliza imetolewa kwa hiyo kama unaweza kujiokoa jiokoe.

MWANDISHI: Kwa hiyo hawa waliokupa taarifa ni wale waliotumwa ama labda ni wasamaria wema?
TUNDU LISSU: Nafikiri kwa jinsi walivyojitambulisha ni wako katika hilo kundi la watu waliotumwa lakini hawakubaliani na mambo haya.

MWANDISHI: Utakuwa hapo hadi lini?
TUNDU LISSU: Nitakuwa hapa mpaka hapo usalama wangu utakapohakikishwa, sipendi kukaa hapa, mimi ni mtu mwenye shughuli nyingi kwa hiyo nataka niondoke hapa haraka iwezekanavyo na bahati mbaya siwezi nikajua itakuwa lini kwa sababu wale wanaopaswa kuhakikisha usalama wangu wanaonekana kama hawataki kujicommit kwamba kama nikitoka nje nitakuwa salama.

MWANDISHI: Kwanini unasema hivyo?
LISSU: Kwa sababu tangu nimekuwa hapa kumekuwa na jitihada za mabalozi wa nchi mbalimbali kuiambia serikali ya Tanzania kwamba haya mambo yanatokea sio masuala sahihi na mpaka sasahivi hizo jitihada hazijafanikiwa bado.

MWANDISHI: Utakapofanikiwa kuondoka, utabakia nchini au utarudi Ubelgiji?
LISSU: Nitaondoka kurudi Ubelgiji kwasababu hali ya usalama sasa hivi sio nzuri hata kidogo, hivi vitisho ni vitu ambavyo lazima nivichukulie kwa uzito mkubwa na wa kipekee.

MWANDISHI: Bado unajiona utasimama tena kwenye kinyang’anyiro kijacho cha Urais na utaendelea na harakati zako za kisiasa?
LISSU: Tuombe Mungu atupe uzima tujue miaka inayokuja itatuweka vipi lakini nachoweza kusema waziwazi ni kwamba harakati ni maisha yangu.