Categories
Siasa

Membe Aongea Na Wanahabari, Asisitiza Kuwa Bado Mgombea Urais kupitia ACT-Wazalendo, Asema “Atafunga Bao Dakika ya 89 Kutokea Benchi.”

Nimewaita kupitia ninyi niongee na Watanzania.

Wengi wameuliza Membe yupo wapi? Au kaunga mkono Juhudi, au kaondoka chama?

Mimi Membe ni Mgombea Halali wa ACT Wazalendo. Ni chama chetu kizuri na nitakipeleka kwenye Uchaguzi wa Mwaka huu kama Mgombea wa Urais.

Kuna watu walikuwa wanasubiri nitamke tu neno ila mambo yatimie.

Mimi hupenda kujibu Maswali.

Hapa nimekuja na Omary Faki Mgombea Mwezi kutoka zanzibar na Meneja Kampeni wa Urais wa ACT.

Ipo nadharia kwamba Vyama vikiungana vinaweza kushinda. Lakini katika bala la Africa, nadhalia hii haijawahi kufanikiwa.

Madikiteta wote wameangushwa na vyama binafsi. Afrika chama kimoja ndo huwa kinashinda sio vilivyoungana.

Vyama 19 bara la afrika vya Ukombozi, vyama 13 vimeshaondoka. Vimeondolewa baada ya vyama vyenyewe kujitafuna na kuwa na mpasuko na vyama vya upinzani vikachukua advantage.

Ili chama Tawala kife, kinatakiwa kipasuke kwanza.

Nadharia ya chama Tawala kupasuka, imeshakomaa Tanzania.

Chama Tawala cha CCM tunakiangusha Mwaka huu kama tutafanya haya nitakayo yasema.

Nini maana ya kupasuka kwa chama. Ni hadi wanachama waseme tumechoka. Angalieni wakati wa kura za maoni za CCM,watu walienguliwa. Sisi ACT tulipokea Applications 42 za kuomba kujiunga na sisi. Sijui walioenda vyama vingine.

Baada ya kura za maoni Bashiru akaanza kuwaahidi kwamba watapewa vyeo watatumbuliwa.

Mimi nlikuwa na wabunge 78 wa CCM, 46 Wamefyekwa na 23 bado wamo CCM. Siwapi majina

Mimi nlijipanga na wenzangu sita ili kushindana na Magufuli, mimi nlikuwa tayari kumkabiri kwenye Uchaguzi na bahati yao walinifukuza.

Hata chama Tawala mambo yanapoharibika wanakimbia. Lazima wapewe sehemu ya kutokea. Anaweza akachagua chama cha kujiunga.

Tunachotaka sisi ni kukipasua chama cha CCM na kimeshapasuka. Sasa aje mtu mwenye nguvu aingie madarakani.

KUSUDIO LANGU

Ndugu zangu watanzania, tumepata tabu sana. Tumepiga kwelikweli. Sasa hivi Tanzania ni Fukara, Watanzania hawana fedha. Dunia haiishi hivi. Dunia ina fedha. Sisi tumerudi miaka ya 80. Serikali haitumii fedha sababu haina kwasababu imekopa sana.

Dunia nzima Serikali ndo tajiri wa kwanza na kuzisambaza. Ukiona nchi haina fedha wa kuajibishwa ni serikali. Serikali ndo mwajiri Mkuu.

Mtu mmoja anasema sasa kama mimi nina fedha kwaninii nikope?

Kopa ulipe kidogo kidogo. Ukienda kununu vitu kwa fedha yako ili uonekane una hela jua unafukarisha Serikali yetu.

Rais aje awe Mimi au Tundu, kazi kubwa itakuwa ni kulipa Madeni. Na mashitaka yote tutakayodaiwa itabidi tulipe.

Tusidanganyane, Serikali hii haona fedha. Tuna ufukara. Na ufukara huu ndo unaofanya watu wakati wa Uchaguzi, Ukichanganya ufukara huu na hasira wakati wa Uchaguzi ndo unawasha moto.

Mimi nmesimamia uchaguzi 19.

Ukichanganya hasira ya kunyimwa haki ukajumlisha na Ufukara walionao ni fujo. Na haya mazingira tumeyatengeneza.

Kwani hatuna njaa? Siku hizi chakula chetu ni mihogo na madafu.
Pale kariakoo unakuta asubuhi anakunywa kahawa, mchana hadi jioni.

Watu wanakula mihogo mibichi na iliyoiva. Wanasisinzia hovyo hovyo

Jana saa nne usiku nimetembelea hotel za dar. Zote ni kiza, hakuna watu.

Jana nmeenda kariakoo nikiwa nmevaa kanzu. Zamani tulikuwa tunaingiza 90 bilioni kwa wiki. Nenda sasa hivi, inatisha. Fremu nyingi sana zimefungwa.

Mtu anasema ukiingia kariakoo na vazi la CCM hawakufanyi kitu kama zamani.

Hawafanyi hivyo sababu wanakuoenda bali ni uoga. Watu hawapo huru.

Uchaguzi huu tuwe na haki. Waangalizi kutoka nje watakuwa wachache. Wale wakubwa wakubwa hawaji. Hawaji sababu wanajua bado kuna COVID-19. Pia UNDP haijatoa fedha sababu Serikali ilikataa fedha za uchaguzi na kwanini walikataa? Muwaulize nyinyi.

Ila wanatakataa sababu ukipokea fedha za UNDP shariti namba moja ni lazima walete international observers. Hawa waliokuja ni Mabalozi na Wafanyabiashara.

Tutakuwa na observers.

Uchaguzi huu lazima itendeke haki.

Pale Zanzibar wanachodai ni haki.

Zanzibar wapo laki nne na sitini elfu tunapiga siku mbili lakini wenzetu wapo Milioni 29 wanapiga siku moja.

ACT wanalalamika kwanini tunaoewa tarehe mbili za Uchaguzi? Ndo maana Maalim seif akafungiwa.

Hatujachelewa kuepusha maafa Zanzibar. Mimi nliona maafa mbele ya Macho yangu Zimbabwe. Ilikuwa hivi hivi kupiga kura mara mbili.

Zimbabwe 2013 walipiga siku mbili ikatokea vita, mwaka 2018 wakapiga kura mara moja.

Zanzibar wameiga hii ya kupiga kura mara Mbili Zimbabwe.

Mimi kama mwanasiasa mbobezi, nawashauri Zanzibar kura ipigwe mara moja.

Wanasema tarehe 27 ni ZEC na tarehe 28 NEC. watu wanahoji, mbona zamani tulikuwa tunapiga kura siku moja?

Ili kukwepa fujo, tuache kupiga kura mara mbili.

Hakuna kitu kibaya kwenye Uchaguzi kama Ukabila na dini.

Nawaomba sana viongozi wetu wa dini, watuunge mkono kimya kimya, wakiendelea kutangaza hadharani, wataingiza nchi kwenye Vita za kidini.

Kama mwanasiasa mbobezi, nawaomba Viongozi wa dini msituongize kwenye vita ya Ukabila na udini.

Kazi ya Viongozi wa dini ni kuhubiri haki amani na Utulivu. Kazi yao ya pili ni kuombea Taifa.

Viongozi wa dini tusiaidieni kuliombea Taifa. Tusihubiri amani na Utulivu bali tuhubiri haki.

Nmefanya utafiti na wenzangu, tumeviona viashiria vya kuwepo machafuko.

Sasa sisikii ile lugha ya tunatest mitambo, mitambo gani? Mitambo yenyewe ishaharibika.

Sisikii ile lugha eti tutashinda asubuhi. Watu wapo kimya kama vile hakuna uchaguzi. Kule mikoani wapo kimya kabisa.

Chama cha mapinduzi hakina fedha. Ndio maana wanaahirisha kampeni. Hivi hamjui kwamba kuna watu wanakidai chama cha mapinduzi tangu 2015? Na hawa wasanii Uchaguzi ukiisha utaanza kusikia naidai CCM.

Nawaomba viongozi wa Dini msiingie kwemye mitego. Tupigieni michepuo chini chini mkienda huko juu mtachafua hali ya hewa

Tulipokonywa Uhuru miaka mitano iliyopita. Jana nlikuwa na sikiliza rais kwenye taarifa yake kwa vyombo vya habari. Clip ya kwanza inazema Waandishi wa habari nipo na ninyi mtakuwa na uhuru clip ya pili inasema Ole wenu.

Wandishi wa habari Mkiogopa mumekwenda na Maji. Unganeni muwe kitu kimoja kuisemea Nchi

Katika Serikali yetu hatuingilia vyombo vya habari.

Sasa hata mabaya yakitokea nchini vyombo vipo kimya.

Wafanyabiasha wakubwa zaidi ya 100 wamefunga biashara. Sasa hivi wafanyabiashara wapo India Mombasa, Lusaka afrika kusini. Kinaniuma ninavyoona hela zilizokuwa zinakuja Kariakoo zipo Lusaka.

Tukiingia Madarakani tutawashawishi warudi nchini.

Wale sio watu wa kudhalilishwa. Ila ni kukaa nao na kuongea

1. Uhuru, Biashara, Kilimo.

Bei ya korosho pamba tumbaku mbaazi sio serikali kuingilia bali iamuliwe na Soko.

Wananchi waambie Bei elekezi ya duniani.

Sisi swala la ajira tunalipa kipaumbele..

ACT tumeweka mbele mambo ya afya. Bima ya afya ya sasa ina ubaguzi

Sisi ACT theluthi mbili itatoka serikalini. Kila watu walipo elfu moja tutajenga Zahanati

Sasa Tanzania imekuwa kisiwa cha mafukara. Haina mahusiano mazuri na Dunia na jumuiya ya kimataifa sababu tumejitenga.

Sisi nchi yetu bado ni fukara. Tuna utajiri ambao upo Kilometa sita kwenda chini ya ardhi.

Tulileta uwekezaji wa bandari ya Bagamoyo, Serikali ya awamu ya tano ikakataa eti ni ina Mkataba mbaya..

Bagamoyo inaleta meli kubwa inabeba makontena milioni moja na laki nane.

Anadai eti watu wakubwa wamegawana.

Stiegler’s gorge sasa kimyaaa.. Wakati zile hela tungezipeleka kwenye gesi.

Sio vibaya kujenga miundombinu. Lakini wewe usiwe rais wa miundombinu kama nyuki. Nyuki ndo kila siku asali.

Rais anataka azitendee Wizara zote 27 sawa. Sio kwenye miundo mbinu tu

Nyuki angegombea urais kwenye animals kingdom tusingemchagua. Nikuchague wewe unatengeneza asali asubuhi hadi jioni? Hapana.