Categories
Habari Siasa

Matumizi Mabaya Ya Fedha za Walipakodi: Magufuli Atuma Ndege Ya Rais Kwenda Kenya Kumleta Mchekeshaji

a

Rais John Magufuli, ambaye kwa miaka mitano ya utawala wake amekuwa akijinasibu kama anayechukia matumizi mabaya ya raslimali za umma, alitoa ndege ya rais kwenda Kenya kumleta mchekeshaji maarufu, Eric Omondi, kwa ziara ya siku mbili.

Kwa mujibu wa taarifa za tovuti ya , licha ya serikali ya Tanzania kupiga marufuku ndege kutoka Kenya, msanii huyo alipewa heshima ya pekee na kulakiwa kwa heshima kubwa.

Akiongea na mtandao huo, Omondi alieleza kuwa ndege ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilimchukua Kenya Agosti 27 na alipofika Tanzania, alipatiwa makazi yenye hadhi ya mwanadiplomasia.

“Ndio, ndege kutoka Kenya zimepigwa marufuku lakini serikali ya Tanzania ilinitumia ndege yake,” alisema msanii huyo.

CHANZO: Kenyans