Categories
Siasa

Fake News: Chadema Watumia Picha Ya Kampeni za Lowassa 2015 Kuonyesha “Mafuriko ya Lissu Shinyanga.”

Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kimeshutumiwa kwa kutumia picha ya kampeni za uchaguzi za mgombea wake wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, Edward Lowassa, kujenga taswira ya umati uliojitokeza kumpokea mgombea wake katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, Tundu Lissu, huko Shinyanga.

Picha hiyo “feki” ilibandikwa kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter na Mwenyekiti wa chama hicho katika mkoa wa kichama wa Kinondoni, Henry Kilewo.

Hata hivyo, picha halisi ni hii ya mwaka Septemba 3 mwaka 2015, mwaka kamili na siku moja kutoka jana.

IMG_20200902_165126.jpg

Miongoni mwa watu maarufu walio- “retweet” twiti hiyo ya Kileo ni pamoja na Kiongozi Mkuu wa chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe, Mbunge maarufu wa Chadema, Halima Mdee, wanaharakati Maria Sarungi na Fatma Karume.

Twiti hiyo bado ipo kwenye akaunti ya Kileo hadi wakati habari hii inachapishwa, takriban masaa 9 baada ya kubandikwa. Hata hivyo, kwa kurejea picha nyingine za mapokezi ya Lissu huko Shinyanga, yayumkinika kutanabaisha kuwa hakukuwa na umuhimu kwa kiongozi huyo mwandamizi wa Chadema kutumia picha feki.

Kwa upande mwingine, Chadema imeendelea kukosolewa kuhusu mapungufu ya wazi ya Idara yake ya Habari iliyo chini ya Tumaini Makene. Kwa mujibu wa mabandiko mbalimbali kwenye mtandao wa kijamii wa Jamii Forums, chama hicho kimeonyesha udhaifu mkubwa katika kurusha matukio ya kampeni za Lissu mubashara na hata mabandiko mitandaoni kuhusu matukio hayo. Moja ya mabandiko hayo ni kama hili lifuatalo

“Anayesimamia Idara ya Habari CHADEMA anakihujumu chama”