Categories
Siasa

Breaking News: Lissu Atangaza Maandamano Nchi Nzima Kushinikiza Tume ya Uchaguzi Kurejesha Wagombea wa Upinzani Walioenguliwa

Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chadema, Tundu Lissu, amewataka Watanzania kufanya maandamano ya amani nchi nzima kuishinikiza Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwarudisha bila masharti wagombea wa vyama vya upinzani walioenguliwa isivyo halali.

Lissu ameongea hayo muda mfupi uliopita wakati anahutubia kwenye uzinduzi wa kampeni za urais, ubunge na udiwani kwa tiketi ya chama hicho, Mbagala jijini Dar es Salaam.

Mwanasiasa huyo ametanabaisha kuwa shinikizo hilo linahusu wagombea wa vyama vyote vya upinzani na si Chadema pekee.

Hotuba ya Lissu inarushwa mubashara HAPA.