Categories
Habari Siasa

Ally Bananga Kupewa u-DC Baada ya Kujiunga na CCM Akitokea Chadema, na Mama Samia Kuahidi “Kumtumia”?

Aliyekuwa mwanachama wa Chadema, Ally Bananga leo Jumapili ametangaza kurejea tena CCM mbele ya Rais Samia Hassan “nawashukuruni vijana wenzangu wa CCM ambao niliwasubiri mje Chadema lakini hamkuja na leo nimerudi nyumbani.”

“Nawaomba wana CCM wenzangu, mniruhusu niwe miongoni mwenu ili tusaidiane na mama yetu katika kuelezea mazuri yanayofanyika na mama, nchi inatabasamu, inapumua,” alisema Bananga, aliyekuwa Diwani wa zamani wa Kata ya Sombetini, Arusha kwa tiketi ya Chadema.

Kwa upande wake, Rais Samia Suluhu aliyempokea Bananga alisema kuwa anamshukuru mwanasiasa huyo. “Namshukuru mwanangu Ally Bananga. Nashukuru sana kwa zawadi hii. Niwaahidi wana Arusha kwamba nitamtumia. Yale yote aliyokuwa anayapigia kelele akiwa kule namrudishia ayafanyie kazi. Karibu sana tujenge nchi,” alisema Mama Rais Samia.

Maoni: Je Bananga atazawadiwa u-DC kama ilivyokuwa kwa wanasiasa wengi wa Chadema waliotimkia CCM? Muda utaongea