Categories
Michezo/Burudani

Senzo Mbaroni Kwa Kuhusika Na Kupanga Matokeo ya Mechi

Taarifa zinaeleza kuwa mshauri mkuu ndani ya Klabu ya Young Africans kwenye mchakato wa kuelekea mabadiliko Senzo Mazingiza Mbatha anashikiliwa na Polisi katika kituo cha Oysterbay jijini Dar es salaa kwa tuhuma za kuihujumu klabu ya Simba SC.

Leo mchana taarifa hizo zilitanabaisha kuwa Mazingiza ambaye alikuwa Mtemdaji Mkuu wa Klabu ya Simba, alifikishwa kwenye kituoni hapo na kuhojiwa kuhusu ishu ya kudaiwa kuwahujumu mabingwa hao wa Tanzania Bara, ili wapate matokeo mabovu kwenye michezo ya Ligi kuu iliyopita.

Mbatha anadaiwa kufanya hivyo kwa kushirikiana na Hashim Mbaga, aliyekuwa mkurugenzi wa mashabiki na wanachama wa klabu ya Simba ambaye naye alifutwa kazi siku kadhaa zilizopita