Categories
Michezo/Burudani

Matatizo Kama Kuni za Kuchochea Mafanikio: Kukimbia “Maisha Ya Kihalifu” Kulivyopeleka Mafanikio ya Kimuziki ya Dababy

 

Moja ya majina makubwa duniani kwenye muziki wa kufokafoka ni rapa Dababy wa Marekani. Msanii huyu ambaye jina lake halisi ni Jonathan Kirk, ni “sura iliyozoeleka” kwenye chaneli mbalimbali za runinga.

Lakini safari ya Dababy haikuwa rahisi. Yayumkinika kusema kuwa aliandamwa na maisha ya “kihalifu” tangu udogoni, na mwaka jana tu alinusurika kwenda jela muda mrefu kufuatia kesi ya mauaji, ambayo kwa bahati nzuri kwake alikutwa hana hatia.

Kilichomnusuru Dababy kutoka kwenye maisha ya “kukimbizana na mkono mrefu wa sheria” ni muziki, kama ambavyo imekuwa kwa wasanii wengi Wamarekani Weusi.

Kuna funzo hapo kwa kila mtu kuwa matatizo yanaweza kuwa kuni za kuchochea mafanikio maishani.