Categories
Michezo/Burudani

CEO Mpya Wa Simba Barbara Gonzalez Aanza Kazi Kwa Ushindi, Simba Wainyuka Ihefu SC 2-1

Image

Afisa Mtendaji Mkuu mpya wa klabu ya Simba, Barbara Gonzalenz, ameanza majukumu yake mapya vizuri baada ya klabu hiyo kuinyuka Ihefu FC mabao 2-1 katika pambano la Ligi Kuu ya Vodacom.

Simba ndio waliokuwa wa kwanza kuona nyavu za wapinzani wao baada ya John Bocco kupachika bao dakika ya 10. Hata hivyo bao hilo halikudumu, ambapo dakika 5 baadaye, Mponda wa Ihefu alisawazisha. Bao la ushindi kwa Simba lilipatikana dakika chache kabla ya kwenda mapumziko, lililofungwa na Mzamiru.

Wakati huohuo, Barbara ameendelea kupokea lundo la salamu za pongezi kutoka kwa wana-Simba wa kada mbalimbali ikiwa ni pamoja na watu kadhaa maarufu. Baadhi ya salamu hizo ni kama zionekanavyo kwenye twiti zifuatazo.

Image