Categories
Maoni Siasa

Maoni: Mama Samia Atazimudu Fitna Za Watanganyika?

Nimekutana na bandiko hili huko Jamii Forums, mwandishi akiwa mtu anayejiita “Boss” nami nimeona lina umuhimu wa kubandikwa hapa tovutini

Ukiwa Rais wa Tanzania hasa kama umetokea Zanzibar..kuna changamoto kubwa mno ya kuyajua makundi ya fitina ya watanganyika na namna ya kupambana na fitna zao..

Rais Mwinyi alikuwa ‘victim’ ‘mkubwa Sana wa makundi haya…ilifikia wakati alikuwa anaona kama mda wa kumaliza Urais unachelewa.

 

Rais akiwa mpole na muungwana na mstaarabu kama walivyo Wazanzibari wengi anaweza kujikuta anachezeshwa ngoma na asijue nani mpigaji wa ngoma hiyo.

 

Yafuatayo ni makundi ya fitina hatari mno. Kwa Rais yeyote anapaswa kuyajua..na kujua namna ya ku-deal nao.

 

1. Viongozi wastaafu:
Hapa Mama Samia ana changamoto kubwa. Hata kama ana support ya Kikwete bado kuna akina Mzee Warioba, Mzee Butiku, Lowassa, Sumaye, Mizengo Pinda, n.k. Hawa Wana makundi yao na watoto wao. Na wana maslahi yao.

2. Team JPM:
Hawa wanajulikana. Advantage ni kuwa ushawishi wao utazidi kupungua lakini wana pose threat bado hasa kama wataunganisha nguvu na makundi mengine.

3. Maaskofu na Baraza la Maaskofu..
Hawa Wana uchungu. Mtoto wao hakumaliza miaka 10. Na inafahamika alivyowadekeza. Samia ategemee waraka na matamko. Sasa wanaona haya tu kum-attack waziwazi kwa sababu ya ukimya waliompa
“mtoto wao” ambae sitashangaa wakimtangaza ‘Mtakatifu’

4. Wana-CCM before JPM:
Hawa ni wale waliozoea ule msemo CCM ina wenyewe. Hawa hasa hasa wanataka tu ‘nafasi za kula’ baada ya JPM kuwaweka pembeni mda mrefu.

5. Wanasiasa wa upinzani hasa wale wanafiki:

Hapa kuna wanasiasa aina wenye maslahi yao binafsi hadi wale wa kutumika na makundi mengine hapo juu. Usishangae kuona mwanasiasa wa upinzani akibeba ajenda za Lowasa au Sumaye kuzipigania.

6. Asasi za kiraia, NGOs:

Hapa napo kuna watumikiao makundi mengine hapo juu. Kuna wanaotumikia taasisi za dini zao. Au hata taasisi za nje. Na kibano cha JPM ndo kitawafanya now waamke kwa nguvu kufidia hasara za miaka ya JPM.
Wengine ni matumbo yao tu ndo wanahangaikia.

7. Wasiotaka Muungano.:
Hawa Kwa upande wa Zanzibar watakuwa kimyaa. Now wataamka wa upande wa Tanganyika. Rais Mwinyi alikumbana na G-55 nusura wamgeuze Gorbachev. Ili mradi Rais ni mzanzibari sasa utasikia kelele zao… na fitina zao.

8. Wenye ndoto za Urais:
Hili kundi nalo limepigika vibaya.
Litajitahidi mno kuchafuana na hata kumchafua Rais mradi waweke mazingira yw wao kuja kuchukua kiti

9. Makahaba wa siasa:
Siku hizi hili kundi linazidi kukua.
Hawana agenda maalum.
Wao popote upepo unapoelekea wapo..
Kimbelembele ndo sifa yao.

10. Waandishi wa habari walionunuliwa:
Katika hayo makundi baadhi yana waandishi wao na vyombo vyao vya habari.

11. ‘Manipulated crowds’
Hayo makundi baadhi hufanikiwa kuzalisha makundi ya watu wengi kusemea agenda zao kupitia media au matamasha ya kiimani.
Tegeemea migomo, maandamano na makelele ya kila aina baada ya mda mfupi tu, hata mwaka usipite.

Chanzo: Jamii Forums

Angalizo: Maoni hayo hayawilishi mtazamo wa “Habari Tanzania.”