Categories
Maoni

Magufuli Kuahidi Ndege 5 Zaidi Akishinda Urais Ni Kiburi na Kuwapuuza Watanzania Wanaolalamikia Ugumu wa Maisha

Screenshot_20200830-050738_1.jpg

Kwamba hali ya maisha ya Watanzania ni ngumu, ni suala lisilohitaji utafiti wala mjadala. Kwamba ugumu huo umechangiwa na serikali kuwa na vipaumbele ambavyo hamvimnufaishi mwanachi wa kawaida moja kwa moja au hapo kwa hapo, nalo si jambo linalohitaji umahiri sana kulielewa.

Ni wazi kuwa mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Rais aliyepo madarakani, John Magufuli, anafahamu fika kuhusu hali ngumu ya maisha inayowakabili mamilioni ya Watanzania. Kadhalika, anatambua fika kuwa japo usafiri wa anga ni muhimu, kuna vipaumbele muhimu zaidi ya hizo ndege.

Lakini kubwa zaidi ni ukweli kwamba hadi sasa ndege hizo hazijazalisha faida yoyote, na taarifa zinaeleza kuwa baadhi ya ndege hizo ni mbovu. Kana kwamba hiyo haitoshi, ununuzi wa ndege hizo sio tu umegubikwa na usiri mkubwa bali pia haufuati taratibu za manunuzi ya bidhaa za umma wala CAG haruhusiwi kukagua hesabu husika.

Moja ya faida za chaguzi ni kuwaadhibu viongozi wenye viburi. Na Watanzania wanaokerwa na kiburi cha Magufuli wana fursa nzuri ya kumfikishia ujumbe kwa njia ya kura hapo Oktoba 28 mwaka huu.

ANGALIZO: Haya ni maoni binafsi na hayaakisi mtazamo wa “Habari Tanzania.”

Picha kwa hisani ya Jamii Forums