Categories
Maisha Maoni Siasa

Uzinduzi wa Kampeni za CCM Dodoma: Makonda Azuiliwa Kwenda Kukaa Jukwaa La VIPs

Chama tawala CCM leo huko Dodoma kimezindua kampeni zake za uchaguzi mkuu kwa nafasi ya urais, ubunge na udiwani. Moja ya matukio yaliyogusa hisia za wengi katika uzinduzi huo ni kitendo cha wanausalama kumzuwia aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, kwenda kwenye jukwaa la wageni maarufu (VIP).

Baadaye, kulisambaa picha inayomwonyesha Makonda akiwa kwenye “jukwaa la watu wa kawaida,” suala lililogusa hisia za watu wengi kwa kuzungatia nafasi yake huko nyuma kama mwanasiasa mwenye nguvu kubwa kabisa nchini Tanzania.

Je hizi ni dalili kuwa mwisho wa mwanasiasa huyo umewadia rasmi? Muda pekee ndio utaongea