Categories
Habari Kimataifa Maisha Siasa

#TIME100: Mama @SuluhuSamia atajwa katika orodha ya mwaka huu ya jarida la kimataifa la TIME ya watu 100 wenye ushawishi mkubwa duniani

Kwanini Mama Samia amestahili kuwemo kwenye orodha hiyo? Anaeleza Rais wa zamani wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf

Rais Samia Suluhu Hassan aliingia madarakani Machi 2021, na uongozi wake umekuwa wa kusisimua. Mwaka huo umeleta mabadiliko makubwa kwa Tanzania. Mlango umefunguliwa kwa mazungumzo kati ya wapinzani wa kisiasa, hatua zimechukuliwa ili kujenga upya imani katika mfumo wa kidemokrasia, juhudi zimefanywa kuongeza uhuru wa vyombo vya habari, na wanawake na wasichana wana mfano mpya wa kuigwa.

Mnamo Septemba 2021, miezi michache tu ya urais wake, Suluhu Hassan alitoa hotuba ya kihistoria kama kiongozi wa tano pekee wa Kiafrika aliyewahi kuhutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Alisimama mahali niliposimama miaka 15 kabla kama Rais wa kwanza mwanamke aliyechaguliwa kidemokrasia barani Afrika.

“Kama Rais wa kwanza mwanamke katika historia ya nchi yangu,” alisema, “mzigo wa matarajio ya kuleta usawa wa kijinsia ni mzito zaidi kwenye mabega yangu.”

Alipozungumza maneno haya yenye nguvu, sikuweza kujizuia kufikiria jinsi mabega ya viongozi wanawake yalivyo na nguvu na ni kiasi gani wanaweza kuleta mabadiliko.

Sirleaf ni Rais wa zamani wa Liberia na mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel